Ziliwahi kusikika tetesi zikiwahusisha marapper wawili wakali wa Bongo Land Tanzania Joh Makinimwamba wa Kaskazini na Mfalme wa Hiphop kutoka kanda ya ziwa jijini Mwanza Fid Q zikidai kuwa wawili hao hawapo kwenye mahusiano mazuri.
Hivi karibuni kumekuwa na matamasha tofauti tofauti ambayo yamekuwa yakiwakutanisha wakali hao na kuwaweka pamoja kwa muda mrefu. Tukianzia kwenye Fiesta, Original Concert jijini Mwanza na hata After Skul Bash na wawili hao wameonekana wakiwa pamoja na kupiga story tofauti na tetesi zilivyokuwa zikidai.
Perfect255 ikaona sio kesi kama ikimvuta karibu mmoja wao na kupiga nae story. Ndipo dodo likamdondokea Joh Makini na haya ndio ambayo alifunguka.
“Me sijawahi kuwa na matatizo na Fid, bali ni fikra tu potofu za watu, labda kutokana na upinzani uliopo kibiashara na mambo ya rap lakini hatuna matatizo, ni mshkaji, tunaongea na kushauriana sometimes kwenye shows na vitu kama hivyo.”
Perfect255 haikusita kumuuliza Joh Makini kuhusu mipango ya kufanya kazi ya pamoja kwa wawili hao na majibu ya Joh yalikuwa “Bado hatujafikiria kuhusu hilo ila naamini ipo siku tutafanya kazi.”
Unaweza kumsikiliza Joh Makini akifunguka mwenyewe kuhusiana na issue hiyo kwa kuplay hii video hapa chini
0 comments:
Post a Comment