Msanii
wa kike aliyewahi kutikisa kupitia muziki wake kwa ufundi wa kukata
viuno akiwa stejini mwanadada Ray C yuko mbioni kurudi tena kwenye game
na tayari ameshafanya ngoma tano na zinatarajiwa kuachiwa hivi karibuni.
eNewz imezungumza
na msemaji wa Wanene Entertainment Gentriez ambapo kwa sasa ndiyo
sehemu ambayo Ray C anatengenezea ngoma zake na amefunguka kuhusu
maendeleo ya Ray C kimuziki na kusema kuwa kwa sasa maendeleo yake ni
mazuri sana na tayari wameweza kutengeneza nyimbo tano za msanii huyo.
“Maendeleo
ni mazuri na sasa hivi Ray C tayari ameshatengeneza ngoma nne kama siyo
tano ambazo tayari zimekamilika tunasubiri tu ziingie sokoni , baada ya
Songa atafata Damian Soul halafu ndio atafuata Ray C”
Wanene
Entertainment wameweza kumsaini Damian Soul na wamesema kuwa bado kuna
wasanii wengine watafuata akiwemo msanii kutoka Kenya ambapo wamedai
kuwa bado wako kwenye mazungumzo.
0 comments:
Post a Comment