Tuesday, December 6, 2016


PNC
Msanii wa muziki nchini, Pancras Ndaki aka PNC ametapeliwa duka na aliyekuwa mpenzi wake na kisha kutokomea kusiko julikana.

Akiongea na Bongo5 Jumatatu hii, PNC amedai duka hilo lilikuwa mtaaa wa Manzese jijini Dar es salaam na alikuwa analimiliki yeye pamoja na mpenzi wake huyo.
“Kusema kweli duka halipo tena kuna mambo yalitokea yule demu wangu niliyekuwa nafanya naye biashara alinitapeli,” alisema PNC.
“Lile duka lilikuwa lakwetu sote, lakini yeye ndiye aliyekuwa akilisimamia. Mimi nipo busy na mambo yangu ya muziki najua yeye anaendelea na duka kumbe amefunga duka na kila nikimpigia simu hapatikani. Nilipoamua kwenda  sehemu ambayo tulifungua hilo duka naambiwa duka liliamishwa,”
Muimbaji huyo amesema tukio hilo limemrudisha nyuma kimaendeleo kwa kuwa duka hilo lilikuwa linamsaidia wakati ambapo hapati show.
Katika hatua nyingine muimbaji huyo amewataka mashabiki wa muziki wake kukaa mkao wa kula kwajili ya ujio wa kazi zake mpya.

0 comments:

Post a Comment