Msanii maarufu kwenye tasnia ya filamu nchini Tanzania Vicent Kigosi maarufu kama Ray,ameshiriki kwenye premier ya filamu nchini zambia.
Premier ya filamu nchini zambia inafahamika kama kwacha,msanii mwingine toka Tanzania alieshiriki kwenye premier hiyo ni Kajala masanja
Akiongea na Perfect255,Ray amesema “nilienjoy sana kushiriki,ulikua muda mzuri sana kwangu kukutana na wasanii wa zambia na kubadilishana uzoefu”
Aidha Ray amesema ameona utofauti wa kiwanda cha filamu Tanzania na cha zambia hasa kwenye ushirikiano baina ya wasanii,Ray amewataka wasanii wa filamu nchini kua na nguvu ya pamoja ili kusogeza tasnia ya filamu mbele zaidi
0 comments:
Post a Comment