News
Huko Twitter kumekucha baada ya Dada wa Waziri wa Rais Magufuli, kuandika ujumbe mzito na mkali sana katika Tweet yake moja huko Twitter,
Mwanadada Mwamvita Makamba amedai yeye kama Mwekezaji binafsi katika
tasnia ya Fashion ametapeliwa na Mbunifu wa Suti matata Bwana Sheria
Ngowi. Ngowi anaesifika sana Africa nzima kwa ubunifu wa mitindo ya nguo mpaka kukubaliwa kumvika nguo Rais wa Zambia, anasadikiwa kumtapeli dada huyo wa Waziri wa Mazingira katika Ofisi ya Waziri Mkuu Mh. January Makamba. Tweet hiyo ilisomeka kama ilivyo hapo juu na kuzua gumzo zito mitandao yote ya kijamii Tanzania kama kulikoni hasa?
SHERIA NGOWI
MWAMVITA MAKAMBA
Hapo alikuwa akimpa taarifa jamaa anayeendesha kipindi kipya mjini
cha Papo Kwa Papo na Papi kinachoruka kila jumatano saa 3 kamili usiku
kupitia YouTube na kinakuwa Mubashara.

0 comments:
Post a Comment