Thursday, December 22, 2016

Mkurugenzi Mtendaji wa Multichoice Tanzania, Maharage Chande (kulia), akizungumza kabla ya kukabidhi msaada huo. Kushoto ni mama mlezi wa kituo hicho, Kuluthum Yusuf.Kampuni ya Multichoice Tanzania imetoa msaada wa vifaa mbalimbali vevye thamani ya shilingi milioni 5 kwenye kituo cha watoto yatima cha Al Madina kilichopo Tandale kwa tumbo, kwa ajili ya mahitaji ya sikukuu ya Krismasi na mwaka mpya. 
Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni hiyo Maharage Chande amesema kuwa wanaushirikiano wa muda mrefu na kituo hicho, ndio maana wameamua kuja kuleta zawadi mbalimbali kwa ajili ya kuwasaidia katika sikukuu pamoja na kuwalipia kodi ya nyumba wanayoishi. “Leo tunatoa vyombo vipya vya kulia chakula,nguo, vyakula pamoja na sare za wanafunzi 50 kwa ajili ya watoto ambao ni wanafunzi”
Kwa upande wake mlezi wa watoto katika kituo hicho Kurutumu Yusuph ameeleza baadhi ya changamoto zinazowakabili katika kituo hicho ni pamoja ulipaji kodi ya nyumba, sare za shule pamoja na ada.Hata hivyo Kurutumu alitoa shukrani zake kwa Multichoice Tanzania kwa kushirikiana nao kwa kipondi kirefu na kuwapatia msaada pale wanapohitaji ili kukidhi changamoto zinazowakabili..
"Ni kweli dstv wanatusaidia kwa mambo mengi hivyo tunawashukuru sana na tunamuomba M/mungu awape moyo wa kuendelea kutusaidia" amesema kuruthumu.
Kituo cha watoto yatima cha Al Madina kina jumla ya watoto 61, wasichana 25 na wavulana 36 kimeanza kupata msaada kutoka katika Kampuni ya Multichoice Tanzania tangu mwaka 2009 hadi sasa ambapo mnamo mwezi wa sita mwaka huu kituo kilipelekewa cherehani 5 kwa ajili ya kujipatia kipato.
Mkurugenzi Mtendaji wa Multichoice Tanzania, Maharage Chande (kushoto), akimkabidhi sare za shule mama mlezi wa kituo hicho, Kuluthum Yusuf.
Bwana Chande akimkabidhi mlezi wa kituo hicho mafuta ya kula. Wengine ni wafanyakazi wa Multichoice Tanzania na watatu kushoto ni Meneja Masoko wa kampuni hiyo, Alpha Joseph.
Mlezi wa kituo hicho, Kuluthum Yusuf (kushoto), akimuonesha nguo zinazotengenezwa na kituo hicho kupitia mradi wao wa ushonaji ambao kwa kiasi kikubwa umetokana na msaada kutoka katika kampuni hiyo ya Multichoice Tanzania.Picha na Dotto Mwaibale.

0 comments:

Post a Comment