Ni ukweli kuwa muziki wa Hip Hop unaanza kupata heshima yake nchini. Baada ya kuonekana utofauti wa muziki wa Mwana FA kwenye nyimbo zake za hivi karibuni, rapper huyo anaanza kusherehekea baada ya video ya wimbo wake mpya kuanza kujitengenezea rekodi zake binafsi.
Imekuwa nijambo zuri kwa wasanii wengi kushukuru mashabiki zao kwa kuwawezesha kupata idadi kadhaa ya views kwenye video zao, hususani Mwana FA ambaye Video ya wimbo wake Dume Surualialiomshirikisha Vanessa Mdee imefikisha zaidi ya views milioni 1 ndani ya wiki mbili na siku nne tangu iwekwe kwenye mtandao wa Youtube. Ni nadra sana kwa msanii anayerap kufikisha idadi hiyo ya views katika kipindi hicho.
Kwa mujibu wa MwanaFA yeye amefarijika sana nakudai, kwa wasanii wengine hiyo sio namba kubwa kwao ila kwake ni big deal kwa sabubu haijawahi kufika kamwe. Kupitia ukurasa wake wa Instagram FA amepost idadi ya views kwenye video yake mpya “Dume Suruali”
Ujumbe wa Mwana FA ulisomeka hivi najua kwa baadhi ya wasanii hii sio namba kubwa hata,ila kwangu its a big deal..sababu HAIJAWAHI kufika kamwe!nawashukuru sana,salutes nyingi,heshima kwenu..ninyoosheni kwa kuifikisha angalau milioni mbili ama tatu nizidi kuwakubali…

…na link sijaitoa kwenye bio mjue hivyo,tafadhali endeleeni kuangalia mnikomoe..


0 comments:
Post a Comment