Siku chache zilizopita zilizuka story kutoka kwa baadhi ya wasanii wa Hiphop Tanzania wakimshutumu hitmaker wa ngoma ya “Pale Kati” Nay wa Mitego kuwa yeye sio mwana Hiphop.
Sasa Perfect255 imemkamata Nay kwenye exclusive interview na kama kawaida yake amewachana kinoma noma wasanii hao na kudai kuwa hawamzidi kwa chochote kuanzia kimuziki hadi kimaisha.
“Nyie ni walala njaa, mimi ukinitoa kwenye list ya walala njaa wala siwezi kulalamika. Hao wanaosema mimi sio mwana Hiphop nipeleke nao kwenye show moja uone nitakavyo wanyoosha.”
Hayo ni machache kati ya mengi ambayo Nay wa Mitego amewatolea wasanii hao, full interview nimekuwekea hapa chini kwenye video hii. Play kumsikia mkali huyo jinsi alivyo wachana wasanii hao.
0 comments:
Post a Comment