Hakika mziki mzuri utabaki kuwa mziki mzuri, na mziki mzuri kupenya ni
rahisi kutoka na uzuri wake. Sasa good news kutoka WCB ni hii hapa.
Kutoka WCB-Wasafi Rich Mavoko na wimbo wake wa Kokoro akiwa
amemshirikisha Diamond Platnumz kwa mara ya kwanza wimbo huo unaingia
kwenye Top 5 ya nyimbo ambazo zinazochezwa zaidi kwenye kituo maarufu
cha BBC Radio 1 Extra.
Kupitia ukurasa wa twitter wa Radio hiyo maarufu kwa Burudani nchini
Uingereza, waliweka Orodha ya wasanii watano ambao nyimbo zao zinachezwa
zaidi, kuwa ni Victoria Kimani kutoka Kenya, AKA kutoka Afrika Kusini,
Kundi la R2Bees kutoka Ghana, Wizkid kutoka Nigeria na Rich Mavoko na
Diamond Platnumz Kutoka Tanzania.
Wasanii wa Tanzania ambao wameshawahi kufanikiwa kuingia kwenye Top 5 ya
Nyimbo zinazochezwa zaidi kwenye kituo hicho ni Diamond Platnumz,
Vanessa Mdee na Ali Kiba.
0 comments:
Post a Comment