Rais
wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, ametuma salamu zake za kuufunga
mwaka 2016 na kuukaribisha mwaka 2017 kwa watanzania, huku akiwataka
kudumisha umoja.
Katika
ujumbe wake alioutuma kupitia mtandao wa Twitter, Rais Magufuli
amewataka watanzania kuendelea kuulinda na kuudumisha umoja katika mwaka
2017.
"Watanzania
wenzangu, tukiwa tunakaribia kuumaliza mwaka 2016, naomba niwatakie
heri ya Mwaka Mpya 2017, Ombi langu kwa Watanzania wote
tuulinde,tuutunze na kuudumisha umoja wetu ktk mwaka 2017 kwa kufanya
kazi kwa bidii. MUNGU IBARIKI TANZANIA."
0 comments:
Post a Comment