Thursday, December 8, 2016

Kwa mwaka 2016, tumeshuhudia muziki wa Hip Hop ukiteka hisia za mashabiki wengi hapa Bongo. Tumeshuhudia kazi nzuri kutoka kwa wasanii kama Fid Q, Stamina, Darassa, Mr Blue, Roma, Mwana FA na wengine kibao.

chemical_tz-20161121-0002
Chemical
Uhaba umeonekana kwa female rappers. Tumewashuhudia akina dada wachache wakitawala kwa mbinde akiwemo Chemical, rapper ambaye anaamini amekuwa chachu ya kuwafanya rappers wengine wa kike kuamini kuwa wanaweza kufanya alichofanya yeye.
Akipiga story na Dizzim Online, Chemical amesema kuwa wengi walikuwa wanaogopa kuingia kwa miguu miwili lakini kwa mwaka huu wameiga nyayo zake na wameonekana.
“Mimi nimetoka kipindi ambacho wasichana wengi walikuwa washaona industry ya Hip Hop kwa upande wa kike labda ishakufa, kwahiyo wengi walikuwa wanaogopa kujaribu. Lakini nashukuru mpaka sasa hivi tunamaliza mwaka washakuja wasichana wengi wanaorap, washaanza kuonekana. Najipongeza kwa kuwa chachu,” amesema Chemical.

0 comments:

Post a Comment