Tumepenyezewa za chini ya carpet kutoka kwenye shirika la wambea Duniani Shilawadu kumuhusu hitmaker wa ngoma ya Furaha Young Dee kuwa yuko hatarini kuwekwa katika mikono ya jeshi la Polisi.
Sababu zinazosemekana kuwa ndio chanzo cha rapper huyo kutafutwa na polisi ni kinachosemekana kuwa amefuta account ya mtandao wa Instagram ya anayesemekana kuwa ni mpenzi wake, bibie Tunda.
Zilisambaa picha katika mitandao ya kijamii zikiwaonyesha maafisa wa polisi wakiwa nyumbani kwa rapper Young Dee na ndipo hapo mizozo ikaanza kuzuka na habari kusambaa kila kona.
.
0 comments:
Post a Comment