Friday, December 30, 2016


Diamond Platnumz na Alikiba ni miongoni mwa mastaa wa Tanzania wanaotajwa kuwa na uhasama ‘Bifu’ lakini hakuna yoyote kati yao aliyewahi kukiri kuwa na tatizo na mwenzake.

Ingawa vyombo vingi vya habari vimekua vikiripoti bifu hiyo kutokana na namna wanavyoishi mastaa hao yani AliKiba pamoja na Diamond.
Rayvanny
Rayvanny ni mmoja kati ya wasanii wanaounda familia ya WCB ambayo iko chini ya Diamond Platnumz mwenyewe, kupitia XXL ya Clouds Fm, Rayvanny aliulizwa kama kuna uwezekano wa yeye kufanya kolabo na Alikiba, Rayvanny alisema….
“Mimi Alikiba nikikutana nae namsalimia tunacheka ananiambia mdogo wangu unafanya kazi nzuri, hatujawahi kuongea sana. Kwa muda mrefu lakini ikitokea siku naweza kufanya nae kwa sababu mwisho wa siku tunafanya muziki na muziki ni biashara mashabiki wanapenda kuona mchanganyiko wa watu tofauti, ikitokea nitafanya nae Alikiba kama kuna mazingira ya kufanya kazi au kolabo tutafanya”.

0 comments:

Post a Comment