Wednesday, December 21, 2016

Ni ukweli usiopingika kuwa wimbo wa Muziki wakwake Darassa ndio wimbo ambao unabamba kinoma noma kwa siku za karibuni.

Kumekuwa na tetesi kitaani kuwa wimbo huo umezifunika ngoma nyingine kibao ambazo zimetoka kwa kipindi cha hivi karibuni, bila kujali ukali wa ngoma hizo lakini wimbo wa Darassa umeonekana kubamba kila kona na kuzifanya ngoma hizo kutodumu kwa muda mrefu kwenye airtime.
Baadhi ya ngoma ambazo zimetajwa kufunikwa na Muziki ya Darassa ni pamoja na Kajiandae wa Ommy Dimpoz na Alikiba na hata Kokoro wa Rich Mavoko na Diamond Platnumz.
Sasa Perfect255 imepiga sroty na hitmaker wa ngoma ya Kokoro Rich Mavoko na amefunguka mengi kuhusiana na tuhuma hizo.
“Kwa mtu ambaye anauelewa muziki vizuri hawezi kuzifananisha hizo nyimbo, zote ni hitsong kimpango wake na kila mtu anafanya kitu chake. Darassa ni mwanamuziki mzuri, uzuri ni mshkaji wangu.” Alisema Rich Mavoko.
Play hii video hapa chini kumsikiliza Rich Mavoko akikusanua ni kitu gani ambacho Darassa amewazidi wana hiphop wenzake na mwisho wa siku ngoma hiyo kuwa hitsong.

0 comments:

Post a Comment