Mchekeshaji Idris Sultan alikutana na swali linalowapa ugumu watu wengi wakiulizwa.
Perfect255 inakusogezea swali hili kwenye kioo chako kama lilivyoulizwa na mtangazaji wa kituo cha redio fulani nchini uganda usiku wa jana kwenye ugawaji wa tuzo za ASFA2016
Kwa upande wako Nani mkali kati ya Kiba na Diamond?, Idris alijibu kama ifuatavyo:-
Wote ni marafiki zangu, lakini sawa, nafikiri wote wanatofautiana, nitajibu kwa kuwatofautisha, sio kama ulivyoniuliza.
Yupi anaimba vizuri? Nitasema Ali Kiba.
Yupi ana ‘hustle’ sana? Nitasema Diamond.
Yupi anapiga hela nyingi? Bila shaka ni Diamond.
Yupi ni mpole, na anauwezekano wa kuingia peponi? Nitasema Ali Kiba.
Alimaliza Idris Sultan alipofanya mazungumzo na mwandishi mmoja nchini Uganda
0 comments:
Post a Comment