Diamond
Platnumz ni mfanyabiashara kwenye muziki asiyeogopa ‘kutake risk’
kwaajili ya kukamilisha azma yake, hata kama uamuzi atakaouchukua
unaweza ukaleta mzozo ndani ya familia yake.
Katika
kunogesha tamasha lake kubwa la Wasafi Beach Party, hitmaker huyo
anamdondosha hasimu mkubwa wa mchumba wake Zari, Huddah Monroe. Kama
umesahau, Huddah aliwahi kuingia kwenye bifu kali na Zari baada ya kudai
kuwa amewahi kutembea na Diamond na kwamba staa huyo ni ‘mali ya umma.’
Diamond ameweka picha ya mrembo huyo kwenye Instagram akiwa ameipa kamera mgongo na kuwataka mashabiki wake kubashiri ni nani.
Katika
kuthibitisha kuwa anakuja, mrembo huyo alipost video Instagram akiiimba
wimbo maarufu wa Darassa, Muziki na kuandika: Coming HOME soon…
Niliota naolewa TZEEE,Single men mkuje kwa wingi tukamilishe ndoto😉
Na blah blah blahhh Sitaki kusikia….😜 Kamwili kangu kanatosha kujigamba..😂 #mistressofalltrades.”


0 comments:
Post a Comment