Kila mpenda burudani weekend hii chimbo ni Jangwani Sea Breez kwenye Wasafi Beach Party siku ya mkesha wa sikukuu ya Christmas ambapo Diamond Platnumz na team yake nzima ya WCB Wasafi wanatarajiwa kutoa burudani siku hiyo.
Mastaa kutoka mataifa tofauti tofauti watajumuika kwenye party hiyo ikiwa hapo awalo tulikwisha tonywa kuwa mrembo Huddah kutoka Kenya na Fabiola kutoka Uganda ni baadhi ya warembo ambao watalinogesha party hilo.
Kubwa kuliko ni leo baada ya Diamond Platnumz kum,tangaza mkali kutoka Nigeria Kcee kuwa kama msanii wa kimataifa atakaye dondoka kwenye show hiyo.
0 comments:
Post a Comment