Wednesday, December 14, 2016

Kutokana na kile kilichodaiwa kuvuja kwa nyimbo ya Diamond ft Neyo “marry you” Diamond alikanusha.

Akiongea kwenye kipindi cha mchana cha XXl cha Clouds fm Diamond alisema “nyimbo haijavuja,ni makubaliano kati yetu na universal kwamba ianze audio kusambaa ili ije kua rahisi video itakapotoka itoboe kama tulivyokusudia”
Haikua rahisi watu kuamini kwasababu nyimbo ilikua ikisikika mtaani,wakati huo huo Diamond hakuwahi kuipost wala kuiongelea.
Hivi karibuni usemi umetimia wa kile alichokisema Diamond kwenye XXL baada ya Neyo kupost namna ya kuununua wimbo huo

0 comments:

Post a Comment