Diamond naamini huwa unachukua muda kuonyesha uwezo wako na nakumbuka kwenye show zako za miaka ya nyuma ilikuwa watu wakisema wazee wa CD macho yote yalikuwa kwako wakiamini LIVE SHOW huwezi ila umedhihilishia umma kuwa ulikuwa unasubiri muda sahihi kwenye nyimbo. kucheza najua wewe ni funiko na juzi tarehe 24 ulidhihilisha hilo na nadhani kila mtu analitambua na hakuna wa kukuzuia lakini juzi katika show yako kuna mapungufu niliyaona. mapungufu yalikuwa ni mengi japo ni ya kawaida likiwepo la poor communication from your DJ Rommy kwenda kwa mameneja wako hadi kusababisha ukazila kuendelea na show. tuachane kwanza na hilo tatizo nitalizungumzia baadae turudi katika suala la uchezaji. Najua wewe ni funiko katika suala zima la kucheza na najua unachokifanya lakini nataka uweke hisia zaidi kwenye nyimbo za huzuni.
Itapendeza sana na utawavutia watu zaidi pale utakapokuwa unaimba nyimbo zako kama NITAREJEA, UKIMWONA ukiwa katika hali ya utulivu wa juu zaidi, uki-win hiki kitu naamini utakuwa unawaliza wengi especially wadada. Na naamini ukiimba nyimbo yako ya KAMWAMBIE katika hali ya utulivu wa majonzi hata wapenzi waliogombana wanaweza kurudiana na ukawa umetoa tiba. Diamond nyimbo za hisia zinataka utulivu na watu kuona kila unachokiimba kinatokea moyoni.mi kwa uelewa wangu mdogo sijawahi hata siku moja kuona dance ya huzuni, instead of dancing labda uwe unapiga chombo chochote cha mziki hata gita. nashukuru kuwa band yako sometimes walikuwa wanajiongeza kwa kupiga beats flani zenye radha ya Ragga lakini na hapo ulipaswa kuweka matendo na si kucheza, hivi inakuja kweli unapoimba "Tatizo kwetu mbagala hapa nyumba mbele jalala" hii direct inaelezea maisha ya chini muhusika aliyonayo halafu eti unacheza hivi kweli mtu atacheza huku anamatatizo. Ngoja nikukumbushe kitu unakumbuka show yako ya january 2015 nchini RWANDA muda ulikuwa umeisha ukawaambia mashabiki naomba kuwaaga" baada ya kuwaaga ukawa umeenda pembeni kidogo ukakaa kisha ukaanza kuimba nyimbo yako ya LALA SALAMA, Kila shabiki yako aliyekuwepo pale alitamani kulia unajua ni kwa nini? Kwa sababu macho na akili zao vilitekwa na utulivu wako, amini nakwambia utulivu wako uliteka hisia zao.
Diamond najua una sababu kubwa kwa nini unajifunza kupiga vyombo vya mziki.. ni kwa sababu unaelekea international levels. huwezi kuwa msanii mkubwa bila kujua kupiga hata gitaa, maana kubwa au lengo harisi la kujifunza kupiga vyombo ni kuteka usikivu mzuri wa mashabiki hasa pale unapoimba nyimbo za hisia. Tamaa yangu kubwa kwako ni kuona unabadilika katika utumbuizaji wa nyimbo za hisia, huwa na-wish nione ukivaa uharisia jukwaani kama unavyofanya kwenye video zako. kwa upande wako nimemaliza kwa sababu katika familia akifeli baba basi jua familia nzima imefeli.
WCB sio Diamond pekee bali hii ni team yenye watu wanaojua nini maana ya mziki biasha, hapo juu lengo langu la kumkosoa Diamond lilikuwa ni kumkosoa baba ili na watoto wasifanye kile kibaya anachokifanya baba. bado nipo pale pale kwenye suala la Show ya tarehe 24. WCB msitake kutuaminisha kwamba wimbo wa huzuni unaweza kupigwa unahuzuni halafu ukaanza kucheza
RAY VANNY
Huyu bwana mdogo naamini anajua nini maana ya mziki na anaju kucheza na akili za mashabiki, waliokuwepo katika show naamini watakubaliana na mimi, wakati akiperform nyimbo ya salome na Diamond kwanza alipaform na LIVE BAND hongera sana kwa hilo, una kila sifa ya kuitwa mwanamziki, una sauti nzuri, unajua kuandika mashairi mazuri na kikubwa zaidi unajua kupiga vyombo vya mziki, bwana mdogo alistopisha band baada ya kuona mashabiki wamezubaa kisha akaanza kuimba nao, niliona Diamond na mameneja wake wakitabasamu maana hawakutegea hicho kitu kwa muda huo, na katika suala la kucheza kwenye nyimbo za huzuni sina sana shida naye maana nyimbo zake bado za kuchezeka.
HARMONIZE
Huyu kijana nyimbo zake zote yeye analia kuumizwa tu, yaani toka ameanza yeye analia tu lakini cha ajabu kwenye show zake ikiwemo na show ya juzi tarehe 24 nilimsikia anaimba "Nitaijutia nafsi yenye kufanya chaguo, chagua la moyo" hapa kwa haraka haraka utaona mtu analalamika na anajuta kwa nini kamkabizi mtu moyo wake na anauchezea, sijui Harmonize ameshajijengea imani ili show iwe nzuri lazima akate mauno. Harmonize kuna wasanii wakubwa hawachezi kwenye show ila wanateka mioyo na hisia za mashabiki, Michael Jackson na kujua kote kucheza kule lakini alikuwa anatulia akifika kwenye nyimbo kama HEAL THE WORLD AU I WILL BE THERE. Angalia nyimbo kama WE ARE THE WORLD" Uliwahi kuona MJ akacheza SHAKING kwenye hizo nyimbo? mfano ulipokuwa unapafomu nyimbo yako ya Matatizo niliona DANCERS wako wanacheza kwa furaha na manjonjo yote, tena wanatoa na tabasabu mwanana hasa pale ulipoimba "simu ya anko Twaha akisema mama yu hio kitandani si wa leo wala wa kesho" hivi unajua huu msitali una ujumbe mzito sana.. mtu unapigiwa simu kuwa mama ako tena mzazi yupo hio hivi utatabasamu kweli? Harmonize hapo ulikuwa unatakiwa ujichukulie point kwa mashabiki zako kwa kuvaa uhusika.
RICH MAVOKO
Mwenyewe kajibatiza jina la Messi wa bongo flava, unajua ana maanisha nini kujiita Messi wa bongo flava? kwa wale wanaofuatili mpira wanaijua kazi ya messi uwanjani, kwa wenzangu na mimi ambao hatufatilii mpira ni kwamba kazi kubwa ya Messi uwanjani ni kupiga vyenga na kuhakikisha anapiga magoli ya kutosha na team inapata ushindi kupitia kipaji chake, au kwa lugha zetu za mtaani tunamuitaga FUNDI, Huyu jamaa sina shaka sana nae sababu nyimbo zake zote ni za ku-bang yaani za kuchezeka Disko isipokuwa tu na yeye huwa anachemka kwenye kupafom nyimbo yake ya SILALI.
HUU NI MTIZAMO WANGU TU,
Frank Movic
+255 654 771 776
+255 654 771 776
0 comments:
Post a Comment