Sunday, December 4, 2016

Jana 09 dec 2016 ilikua siku poa kwa star wa hit single ya “kajiandae” Alikiba kwenye ugawaji wa tuzo za AbryanzStyleAndFashionAwards(ASFAs2016) zilizotolewa Kampala Serena Hotel
Alikiba kafanikiwa kuondoka na tuzo mbili ikiwemo ya most stylish artiste East Africa na most fashionable music video,ambapo most fashionable music video ni video ya aje
Huu umekua mwendelezo mzuri kwa msanii Alikiba kuufanya muziki wake kupenya nje ya mipaka ya bongo,
Perfect255 imeongea na baadhi ya mashabiki juu ya mtazamo wao kwenye ugawaji wa tuzo hizi
“Kwajina naitwa Kareem Nditu wa Gongo la mboto,kwa ujumla mchakato wa upigaji kura ulikua wazi sana na mwepesi,kuhusu kupata tuzo mbili kwa msanii kama Alikiba binafsi naona anastahili kwasababu anamashabiki wa kutosha”
Mwingine ni Maria Funga wa mbagala kizuiani “Alikiba anastahili asilimia mia kwasababu kiba ni kipenzi cha watu”alimalizia shabiki huyo.
Idris sultan mchekeshaji kutoka Tanzania ndie alikua host wa tuzo hizo za ASFSs2016

0 comments:

Post a Comment