Wednesday, December 28, 2016

Wikiendi iliyopita ilitengenezwa historia Dar es salaam kwa kundi la WCB kufanya show kubwa pembeni ya fukwe za bahari ya hindi maeneo ya Jangwani Sea Breeze na kualikwa baadhi ya mastaa mbalimbali akiwemo Vera Sidika toka Kenya ambaye alikua miongoni mwa Host wa Beach Party hiyo.
Vera Sidika

Kwenye mtandao wa kijamii wa Snapchat Vera Sidika ameonekana akishangazwa na namna ambavyo wahudhuriaji wa party hiyo walivyovaa mavazi ambayo sio rasmi sana kwa ajili ya beach, Vera ameandika “I wonder was I the only one dressed for the occasion at Wasafi Beach Party people dressed in suits,club dresses, denim jeans, jacket. I’m lost. Whats’s the meaning of beach party if you look the same you would on normal club night”.

Mbali na hilo Vera na mrembo mwingine wa Uganda, Anita Fabiola alitisha sana usiku huo.

0 comments:

Post a Comment