Wednesday, December 14, 2016

Afisa Mkuu wa Masoko wa Vodacom Tanzania, Ashutosh Tiwary (kushoto) na Mkuu wa Masoko na Mawasiliano, Nandi Mwiyombella (kulia) wakimsikiliza Afisa Mkuu wa Idara ya Mawasiliano na Uhusiano wa Kampuni hiyo, Rosalynn Mworia(katikati)akifafanua jambo kwa waandishi wa habari
Wateja wa Vodacom Tanzania wameletewa promosheni mpya inayojulikana kama ‘Nogesha Upendo’ ambayo itawawezesha wateja wake kujishindia zawadi ya fedha taslimu, muda wa bure wa maongezi na MB za Interneti kila siku katika msimu huu wa sikukuu.
Zawadi zenye thamani ya shilingi Bilioni 5 zitatolewa kwa wateja wapatao 500 wataoweza kujishindia shilingi milioni 1 kila mmoja katika kipindi chote cha msimu wa promosheni.
Akiongea katika uzinduzi huo, Afisa Mtendaji Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano Vodacom Tanzania, Rosalynn Mworia alisema kila mteja wa Vodacom ana nafasi ya kujishindia zawadi mbalimbali.
“Vodacom Tanzania tunayo furaja kuzindua promosheni ya msimu wa sikukuu ya ‘Nogesha Upendo’ inayolenga kuleta shamrashamra za furaha ya sikukuu kwa wateja wetu. Tunajua sikukuu hizi zinaleta familia za kitanzania na marafiki pamoja kufurahi na kutumiana salamu za upendo,tumeleta promosheni hii kwa ajili ya kuwazadia wateja wetu wote kila wanaponunua vifurushi vya muda wa maongezi na Data kila siku.”
Pia alisema promosheni hii itawezesha wateja 500 kujishindia kila mmoja shilingi milioni 1 katika droo za wiki na wengine watajishindia shilingi 100,000 katika droo za kila siku katika msimu huu wa sikukuu kupitia promosheni hiyo.
“Mbali na wateja kujishindia dakika tano za muda wa bure wa maongezi na kuperuzi internet, wateja wa Vodacom pia kila watakaponunua vifurushi wataingizwa kwenye droo za kila siku na kila wiki za kujishindia vitita vya fedha. Kiasi cha shilingi milioni 700 zimetengwa kwa ajili ya kuwazawadia wateja wetu katika msimu huu wote wa sikuu”. alisema Mworia.
Baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya kuzinduliwa rasmi Promosheni ya Nogesha Upendo leo jijini Dar es Salaam.
Kwa ujumla,Vodacom imetenga zawadi zenye thamani ya zaidi ya shilingi Bilioni 5/- kwa ajili ya kuzawadia wateja wake kwa njia ya fedha taslimu,muda wa maongezi na bando za intaneti(MB).
Promosheni hii itakadumu kwa kipindi cha miezi 2 kuanzia Jumanne hii kwa ajili ya wateja wote wa Vodacom ambao laini zao ziko hewani na watakanunua vifurushi vya kupata huduma mbalimbali za kampuni hiyo.
“Promosheni ya Nogesha Upendo imebuniwa ka ajili ya kuwashukuru wateja wetu kwa kutuunga mkono muda wote. Tunawatakia heri katika msimu wa sikukuu na tunawakumbusha wakati wote kufuatilia zawadi watakazokuwa wanazishindia kutoka mtandao wa Vodacom kuanzia muda wa maongezi na fedha taslimu zitakazowawezesha kufurahia sikukuu pamoja na familia zao na marafiki. Hivi ndivyo Vodacom tumejizatiti kufanya maisha ya wateja wetu kuwa murua na kusambaza upendo.” alisisitiza Mworia
Kwa upande wa mmoja kati ya wateja ambao walihudhuria uzinduzi huo na kujaribu kujiunga na kifurushi cha Vodacom na kujishindia zawadi mbalimbali, alieleza jinsi walivyoipokea promosheni hiyo.
“Kusema kweli hii promosheni nimeipenda sana kwa sababu inakuza zaidi ya kile unachokinunua, kama hapa nimenunua kifurushi cha tsh 2000 nipepata dakika zakutoka pamoja na MB za internet. Kwa hiyo mimi binafsi naifurahia hii huduma kwa sababu imekuja wakati muhafaka,” alisema mteja huyo aliyejitambulisha kwa jina la Christopher Abass.

0 comments:

Post a Comment