WAANDISHI wa habari watano wanusurika kifo baada ya gari walilokuwa wamepanda kupata ajali wakiwa kwenye msafara wa Naibu Waziri wa Nishati na Madini wilaya ya Nyasa. Ajali hiyo ilitokea jana, ambapo gari walilopanda Toyota Land Cruser kupinduka na kutumbukia mtoni. Waandishi hao ni Emmanuel Msigwa Azam Tv, Joseph Mwambije ITV, Adam Nindi Star tv, Amon Mtega Mtanzania na Noela Njawa TBC. Hali zao zinaendelea vizuri.


0 comments:
Post a Comment