Mziki wa bongo flava unazidi kukua siku hadi siku na huu ni ukweli usipingika kuwa bongo flava ndio mziki unaokuja kwa kasi sana barani afrika, lakini mziki huu usingekuwa na nafasi ya kutambulika katika anga za kimataifa kama sio juhudi za wasanii na wadau kadhaa wa mziki huu.
Watanzania wanne wameshinda tuzo za WAMVA TV. WAMVA ni kituo kikubwa cha TV cha nchini ghan. Kituo hicho leo kimewatangaza washindi watuzo hizo katika ukumbi wa LIZZY SPORTS COMPLEX uliopo katika mji wa Accra. Ni washindi 22 tu waliopatikana kati ya 170 waliokuwa wanachuana katika tuzo hizo.
Waandaaji wa WatsUp TV Africa Music Video Awards (WAMVA) wametangaza washindi wa tuzo hizo lengo lao likiwa ni kuongeza na kuhimiza uzalishaji wa video bora za muziki barani Afrika na kwingineko.
Kwa kifupi washindi walitangazwa katika hafla iliofanyika katika ukumbi waLizzy Sports Complex mjini Accra, washindi 22 walipatikana kati ya washiriki zaidi ya 170 wakiwemo na waongozaji wa video toka nchi mbali mbali.
Kura ya "Video bora ya Mwaka" imeenda katika video ya "Kidogo", kwa Diamond Platnumz kutoka Tanzania akishirikiana na P-Square na iliyoongozwa na Godfather.
Godfather pia alishinda "Muongozaji bora wa mwaka" kupitia video ya "Kidogo".
Washindi wote wamepatikana kwa kupigiwa kura toka pande zote duniani na wote walioshinda watashiriki katika tamasha la mwaka ujao lijulikanalo kama "MADE IN AFRICA CONCERT"
Angalia orodha kamili ya washindi hapa chini.
Best Newcomer Video of the Year
Hamonize – Bado feat. Diamond Platinium (Tanzania)
Best African Reggae Dancehall Video
Shatta Wale - Chop Kiss (Ghana)
Best Afro Pop Video
Scientific - Rotate feat. Quincy B (Liberia)
Best African Hip-hop Video
Iba One - Dokera (Mali)
Best African RnB Video
Alikiba - Aje (Tanzania)
Best African Traditional Video
Tay Grin - Chipapapa feat. 2 Baba (Malawi)
Best African Dance Video
Oudy 1er – Lokolo (Guinea)
Best African Collabo Video
Diamond - Make We Sing feat. AKA (Tanzania)
Best African Group Video
Navy Kenzo - Kamatia (Tanzania)
Best African Male Video
Diamond Platinium - Kidogo feat. P-Square (Tanzania)
Best African Female Video
Vivian Chidid – Wuyuma (Senegal)
Best African Performance
DJ Arafat - Concert a Korkogo (Cote D’Ivoire)
Best International Video
Beyonce - Formation (USA)
Best East African Video
Alikiba - Aje (Tanzania)
Best Central African Video
Ferre Gola - Tucheze feat. Voctoria Kimani (DR Congo)
Best North Africa Video
Ibtissam Tiskat – Ma Fi mn Habibi (Morroco)
Best South African Video
Casper Nyvorvest - War Ready (South Africa)
West Africa Video
DJ Arafat – Maplorly (Cote d’Ivoire)
Best African Video Director
Kidigo (Nigeria)
Best African Music of the Year
Diamond Platinium – Kidigo feat. P-Square (Tanzania)
Special Recognition Award Music Video Africa
Mr Eazi - Skin Tight feat. Efya (Nigeria)
Viewer’s Choice Awards
Designer - Panda (USA)

0 comments:
Post a Comment