Tukiwa tumekaribia kufunga mwaka, tumeona wasanii wengi wa rap na Hip Hop wakijitahidi sana na kurelease nyimbo kali na zenye ubora wa hali ya juu kuliko hapo awali. Hapa nazungumzia nyimbo kama Dume Suruali, Muziki na Astara Vaste
Kuna mijadala mingi inaendelea kuhusu ni nani msanii wa kwanza kufikisha views milioni moja katika YouTube, ila leo mimi ningependa kuongelea contribution ya Azma katika Hip Hop ya Tanzania.
Azma Mponda si jina geni kwa watu wote wanaofuatilia historia ya muziki wa kizazi kipya, amekuwa kwenye muziki kwa kipindi kirefu na amefanya mambo mengi. Azma ameanza kupenya masikioni mwa watu tangu mwaka 2008 alipoachia nyimbo kama My Name Is Hip Hop, Bongo Flava inakufa nk.
Aidha Azma alipata kujulikana zaidi mwaka 2013, baada ya kuachia wimbo wa Kipimo Cha Penzi, ambao inasemeka ni wimbo bora wa mapenzi kuwahi kutokea. Ukisikiliza hata leo, utahisi ni wimbo mpya kutokana na maudhi yake. Hii imepelekea wasanii wengi kama Belle 9 kumzungumzia Azma kama mwanamuziki bora mwenye uwezo wa kuandika nyimbo za mapenzi, na msanii Chindo alidiriki kumfananisha Azma na mwanamuziki LL Cool J wa Marekani.
Kwa upande wa wasanii wakongwe kama Profesa Jay na Fid Q wamewahi kumuelezea AZMA kama msanii bora ambaye hapewi heshima anayostahili. Profesa Jay alimpandisha Azma kwenye show ya Kili music tour mjini Kahama na kutumia zaidi ya dakika tano kumuongelea na kumpa nafasi ya kuimba. Mtangazaji wa zamani wa Victoria FM, Josefly na mwana habari mkongwe Fredrick Bundala (Skywalker) wamewahi kumzungumzia Azma kuwa miongoni mwa wasanii kumi wanaOchukuliwa kawaida na wadau wa muziki wakati ana uwezo mkubwa sana
rejea.
rejea.
Hata hivyo umaarufu wa Azma ulianza kuongezeka sana mwaka 2014 na 2015 baada ya kuachia nyimbo kama Kuwa na Azma, Utata wa Katiba nk. Wimbo uliomfanya Azma akatambulika zaidi ni wimbo wake wa Jinsi ya kumfikisha mpenzi, ambao ulimpa umaarufu sana kwenye mitandao ya kijamii. Wimbo huu ulipelekea Azma kuwa msanii wa kwanza wa Hip Hop kufikisha views milioni moja Youtube.

0 comments:
Post a Comment