Monday, December 5, 2016


Ziara ya Waziri Mkuu katika Jiji la Arusha imefuta machozi ya watu wa arusha kwa kutatua kero sugu za wananchi jijji humo




katika ziara hiyo ya siku tatu jiji humo Majaliwa ikiwa ni eneo la kwanza la ziara yake ambapo alifanyakazi mpaka usiku kwa kukutana na watumishi mbalimbali pamoja na wafanyabishara na walimu  mpaka usiku kupitia vikao mbalimbali ulivyofanya Na watumishi, walimu pamoja Na wafanyabiashara.

 Majaliwa amefanikiwa kuurejesha uwanja namba 68 kilichopo kwa Lovolosi kwa umma kutoka kwa watu wachache waliokipora kwa maslahi yao. ameagiza kiwanja hicho kitumike kama soko kwa ajili ya wafanya biashara wadogowadogo (machinga) na matumizi mengine ya umma.
Waziri Mkuu Majaliwa  ametatua changamoto ya muda mrefu kwa  wakazi wa Arusha na umezindua mpango wa kuwainua vijana Kiuchumi sambamba Na kuwapatia Kadi za Afya ya jamii. 


hata hivyo amewafungukiwa milango kwa wasafirisha abiria ndani na nje mji huo kPia Waendesha Noah sasa watapata Lesseni ya kusafirisha abiria Kwa umbali zaidi ya Km 50 


Majaliwa  amezindua mpango wa kihistoria wa kuwawezesha vijana kwa kuwapatia boda boda za mikopo isiyo na riba kwa vijana 200 zilizogharimu Tshs milioni 400 ikiwemo za walemavu 3 haya ni matunda ya Jitihada za Mkuu wa Mkoa Arusha Mh Mrisho Gambo kwa kutumia wadau wa Arusha.


Aidha, ametoa Kadi za bima kwa vijana wengine wa bodaboda 250 zilizolipiwa na Mbunge wa Viti Maalumu Mh Catherine Magige.

Wakati huo huo Waziri Majliwa amemuagiza Mkurugenzi wa Jiji la Arusha kuchukua hatua kwa Wafanyabiashara waliojikwapulia vibanda katika maeneo ya Stendi ndogo, Soko Kuu Na Kilombero bila kufuata taratibu za manunuzi.


0 comments:

Post a Comment