Diamond na WCB kwa ujumla wameahidi kutoa msaada wa nyumba tano kwa wakazi wa Iringa kufuatia mafuriko yaliyotokea na kusababisha uvunjifu wa nyumba 86.
Diamond kaandika hayo kupitia ukurasa wake wa instagram alipotembelewa na mkuu wa wilaya ya Iringa mjini mh:Richard Kasesela.
Diamond katumia fursa hiyo kumshukuru mkuu wa wilaya huyo kwa kuwatembelea ofisini kwao,aidha Diamond katumia nafasi hiyo kuwataka watanzania wote kuchangia chochote kwa wakazi wa Iringa waliopotelewa na makazi wapate hifadhi.
Nukuu ya alichokiandika Diamond
” lakini pia nitumie fursa hii kuwapa pole ndugu zetu wa IRINGA kwa kubomokewa ama kupoteza makazi zaidi ya 86 kutokana na Mafuriko yaliyotokea….kwakuamini kuwa sisi sote ni binaadam na kuwa la kwako ni sawa na la kwangu, tukiwa kama @Wcb_Wasafi tumeahidi kutoa Nyumba Tano kwajili ya wahanga hao na Panapo Majaaliwa tutazikabidhi Nyumba hizo siku tutayofika Iringa
….. ndugu zetu wapendwa kwa alie na chochote pia anaweza kuwachangia ndugu zetu wa Iringa, waweze fanikisha makazi ama Nyumba hizo 86..”
0 comments:
Post a Comment