Wednesday, December 28, 2016


Ni 16 flani hivi ina malizia kuchukua time yake, so tunaelekea ukingoni. Bado yapo mambo mengi yanayo hesabiwa kabla ya kuumaliza mwaka.

Miongoni mwa mambo yaliyowekwa kwenye uzani mmoja ni uhasama au ugomvi (Bifu) kati ya Wasanii dhidi ya Wasanii wenzao. Baada ya kuona Watayarishaji (Producers) waliofanya vizuri 2016, Jana  kupitia kipindi cha XXL cha Clouds Fm wametaja bifu hizo.
  1. Diamond & AliKiba
Beef ya washkaji zetu ina miaka zaidi ya mitatu, na haimaliziki sana sana mwaka huu kiba kwenye interview aliyofanya na media ya kenya citizen tv na radio, alilalamika kuwa amehujumiwa na manager wa diamond sallam sk, kwa kumfanyia fitina za kumzimia mic ktk show moja iliyofanyika mombasa
2. Diamond & Ommy Dimpoz
Hawa walikua marafiki wakubwa sana na wana kama miaka miwili hawa roll pamoja, kukawa kunasemekana kuwa kuna beef lakini hakuna hata mmoja kati yao aliyefunguka mpaka juzi kati Diamond alipoweka wazi hisia zake, ishu za kupumiliana na nini, baadae Dimpoz akapangua shuti na kulalamika kuwa alijipendekeza kwa mchizi lakini hakuwa ana fanyiwa fair na diamond
3. Man Fongo & Sholo Mwamba
Beef ya Manfongo na Sholo Mwamba hawa washkaji zetu wana historia ya kuwa washkaji kinoma noma na enzi hizo Sholo Mwamba anaimba vigodoro dj wake alikua Manfongo, kutokana na Sholo kuwa na kiki kubwa akawa anapata booking nyingi za kuperform hadi mikoani, lakini kutokana na dau analopewa kuwa dogo akawa anashindwa kusafiri na dj wake ambae ni manfongo.
So Manfongo akawa anabaki town bila mchongo coz mziki boss wao anao, lakini hakuna performer ndo Manfongo na yeye akaanza ku hype kwenye visingeli, baadae Sholo mwamba akapata label, akaishtua management kuwa kuna kichwa kingine mtaani ambacho ni Manfongo, ikaja ikatokea Sholo akaimwaga ile label kutokana na management kuwa inampendelea Manfongo, utata ukaanzia hapo, baadae wakakutana kwenye tour bus ya fiesta kuna maneno yalisemwa kuhusu Wema Sepetu taarifa zikamfikia mama Wema, bimkubwa akatoa mapovu yake kwa Fongo kwani alifikishiwa taarifa kuwa Manfongo ndo alikua anamsema, Fongo akamtuhumu Sholo kuwa ndo alimsingizia maneno beef likawa kubwa.
4. Diamond & Wema Sepetu
Wawili hawa waliowahi kuwa wapenzi walikua na beef ya chini chini tangu waachane, lakini mwaka huu waliwashangaza watu kwa kuimaliza kiutu uzima kwenye birthday zao walipostiana na Wema kumwombea kura Diamond kwenye tuzo za kimatiafa alizotajwa mwaka huu, lakini pia beef ya Aunty ezekiel na Wema ikaishia hapo hapo.
5. Young D & Mtu Chee
Kulitokea vuta nikuvute kati yao, baada ya Young d kuchomoa kushiriki kwenye project za Mtu Chee kwa madai kuwa eti hawako serious, mapovu yakawatoka upande wa pili mpaka Max ambaye ni manager wa Young d kipindi hiyo walikua wametofautiana akaingilia kati kwa kulipia video ya Mtu Chee design kumwonyesha Young D kuwa Mtu Chee wako serious ila yeye anazingua, jamaa sasa hivi wameyamaliza wako viziri na Young D yupo under management ya MDB ya Max.
6. GodZilla & Bill Nas
Kwanza wamesoma chuo kimoja Cbe, beef yao ilianza kama utani kwa watu kuwalinganisha kuwa uchanaji wao unafanana, hiyo kitu ilienda kwa zaidi ya mwaka, sasa kuna siku mida ya usiku zilla alitoa surprise ya mapovu dhidi ya Billnass kwa kuelezea kuwa Billnenga ni wack, eti alikua anamfata room kwake pale kuomba msaada wa kufundishwa kuandika na kuchana, akaandika kuwa nenga anapenga, vitu kibao na Billnenga akajibu kwa kusema kuwa ni kweli alikua anamfata zilla room ili kujifunza game ukizingatia ametanguliwa kwenye game, na kuhusu kupenga akajibu mteja anawezaje kuwa na maendeleo kama yeye? Kwamba yeye ana malengo na lazima yatatimia.
7. TID & Dully Sykes
Mwaka huu Tid ali release ngoma yake ya confidence ft Dully sykes na Joh makini, bonge la ngoma, lakini baadae Tid akaja kulalamika kuwa Dully alikataa Joh makini kushirikishwa kwenye ngoma hiyo, lakini Tid anasema ye akamwita Joh, baadae ngoma ikafanya vizuri eti Dully aka kataa kufanya video, ndo mapovu yakamtoka sana Tid, Dully alikua hataki kumjibu kabisa Tid na jibu kubwa alilokua anatoa kuwa Tid mnamjua.
8. Young D & Dogo Janja
Washkaji zetu hawa hawana historia ya kuwa na beef, ila Janjaro alianza kwa kum diss kwenye ngoma yake ya My life nanukuu “kitambo mi nachana zaidi ya wanyamwezi mtaongea sana nyie ma young hamniwez, mtazidi kupenga kisa stress mpaka totoro, nawanyima chakula mwaka mle magodoro”, baade Young D alikuja kuimaliza beef kwa kusema ameiskia ngoma kali inafanya vizuri.
9. Country Boy & Quick Rocka
Mwezi March mwaka huu, rapper Country boy alitokwa na povu dhidi ya Quick rocka, hiyo inatokana na kauli ya Quick kwenye interview na xxl kuwa kundi la Omg ni generation mpya ya Rockaz, ndo Country akaibuka na kudai kuwa Omg sio sehemu ya Rockaz ila Omg ni kundi la wasanii wanaojitegemea na yeye Country ndio aliyewaunga na kuwapiga tough kuingia kwenye mainstream ya Bongo flava.
10. Ney Wa Mitego (Kuwachana Wasanii wenzake kwenye ngoma yake)
Beef na wasanii wenzake baada ya kuwaimba kwenye Shika adabu yako, aliowataja ni actor Niva kuwa hana nyumba analala kwenye gari, Ray kigosi anatumia mkorogo, Wema sepetu ali fake kibendi, Shetta anapewa magari na Chief kiumbe na sio yake vitu vitu vingi na wasanii wengine walimjibu wengine wakaimaliza kwa kuchuna au kucheka kama comedy.
11. Chalz Baba & Khalid Chokoraa
Beef yao washkaji zetu ni ishu za kuchapiana, na hiyo ilikuja kujulikana baada ya Chokoraa kulalamika kuwa Chalz baba amepita na mchumba wake ambae alikua amepanga kumuoa, na amefanya hivyo maksudi huku akijua swahiba wake anataka kufunga ndoa na shemela, ktk kupanic Chokoraa akaahidi kuwa ataoa hivyo hivyo coz amesha changisha michango zaidi ya milioni 10, huku na huku ndoa haikufanyika tena.
12. Shilole & Vanessa mdee
Hii tunaweza kuita bifu ya kutengeneza ambayo iliwashangaza watu wengi ingawa baadhi yao walikua wakimdharau Vanessa mdee kuingia kwenye beef na Shilole huku wakimwambia Vanessa ana shule na msanii wa kimataifa hana sababu ya kubishana na Shilole lakini hawa beef yao ilikua ya kutenegenza na wakaja kupiga bonge la show club billcanas.
Nambie bifu ipi uliyoielewa kwa mwaka 2016 kati ya hizo 12 na kui-reason kidogo bifu hiyo.. uwanja wa coments ni wako.

0 comments:

Post a Comment