Mwanafunzi
wa Chuo kikuu kimoja cha China ambaye jina lake halikutambulika kwa
haraka ameamua kufanya ‘uchizi’ ili mradi tu aipate pesa ya kununua aina
mpya ya iPhone iliyoingia sokoni, iPhone6.
Katika
tangazo hilo kijana huyo anaeleza kuwa yuko tayari kumkodisha mpenzi
wake kwa mtu yeyote atakayeweza kutoa pesa ili jamaa apate kiasi cha
kutosha kuinunua iPhone 6 yenye screen kubwa.
Picha ya kijana huyo imesambaa kwa kasi katika mtandao wa kijamii unaotumiwa na wachina uitwao ‘Weibo’ ambao ni kama Twitter.
Tangazo
hilo limeambatana na picha za mpenzi wake na amewatoa hofu wateja
wanaosita kuingia nae mkataba kuwa hata mpenzi wake ameridhia na yuko
tayari kudate na mtu yeyote atakaejitokeza.
Muda
wa kuwa na msichana huyo baada ya kumkodi umebainishwa kutokana na
malipo yatakayofanywa na mteja. Viwango ni vya saa 1 (10 yuan), siku 1
(50 yuan) au mwezi mmoja (500 yuan).
Hata
hivyo, wapenzi hawa sio wa kwanza kujiweka sokoni ili wapate bidhaa ya
kampuni ya Apple. Mwaka jana katika uzinduzi wa iPhone 5, wanandoa wa
Shaghai waliwaweka sokoni watoto wao watatu ili wapate pesa ya kununua
computer na simu za iphones lakini walikamatwa na kufunguliwa mashitaka.
Lakini pia kijana mdogo wa Hunan alijitolea kuuza figo lake ili apate pesa ya kununua iPad na iPhone.
Siyo
hayo tu, hivi karibuni mwanaume mmoja wa Saudi Arabia ametaka kupewa
iPhone 6 kama mahari ya dada yake hata kabla aina hiyo ya simu
haijazinduliwa Bahrain.

0 comments:
Post a Comment