Monday, January 9, 2017

Ikiwa suala la wasanii kuwa na lebo zao linaendelea kushika hatam msanii Barnaba Boy ametusanua baadhi ya vitu ambavyo hawezi kuvifanya katika lebo yake ya Hightable Sound.

Akiongea na Perfect255 Barnaba Boy amefunguka kuwa hana plan ya kumsaini msanii mkubwa, lakini plani yake ni ku-deal na watu wenye vipaji ambao anawasaidia na mwisho wa siku waje kuwa wakubwa ili kuongeza idadi ya wasanii kwenye industry ya muziki hapa Bongo.
“Mimi sina plan ya kuja kumsaini msanii mkubwa, kabisa kiukweli plani yangu ni kuzalisha products ambazoo zitakuja kuwa kubwa, labda ikitokea msanii mwenyewe ndio apende kujiunga na team yangu au misaada mingine hapo nitasaidia lakini sio kumchukua msanii na kumsimamia kama manager.”
Unaweza kumsikiliza Barnaba akifunguka mwanzo hadi mwisho kuhusiana na issue hiyo kwa kuplay hii video hapa chini.

0 comments:

Post a Comment