Mwanamme anayejiita Beach Boy akiendelea kumfundisha dada mmoja kuogelea.
Beach Boy akiwa kamkumbatia dada huyo.
Baadhi
ya mabinti na wanawake wengine wanaofika kwenye Ufukwe wa Coco uliopo
Oysterbay jijini Dar kwa lengo la kufundishwa kuogelea, wamekuwa
wakijikuta wanafanyiwa vitendo vichafu, ikiwemo kubakwa na wanaume
wanaojiita Beach Boys, Risasi Mchanganyiko lina mkanda kamili.
INAKUAJE?
Akisimulia
mchezo mzima unavyokuwa, kijana mmoja ambaye ni mwenyeji wa maeneo hayo
alisema: “Watu wanapokwenda beach, wasichana wengi wanapenda kuogelea
na wengi wao hawajui, hivyo wale Beach Boys wanaokodisha maboya huingia
nao kwenye maji kwa lengo la kuwafundisha.
“Kinachofuata sasa, Beach
Boys hupeleka boya hadi kwenye kina kirefu, wakifika huko kijana huomba
apewe penzi huku akimtishia mdada kuwa akigoma anamuachia afe.
“Mdada
akijifanya mbishi anazamishwa, anakunwya maji kidogo kisha anaibuliwa,
akishaona mlango wa kuzimu anakubali kiulainii. Kwa staili hii wadada
wengi wamepewa mimba na kuambukizwa magonjwa.”
MSIKIE MHANGA
Mmoja
wa mabinti aliyewahi kufanyiwa mchezo huo aliyeomba hifadhi ya jina
lake alidai kuwa, kuna wakati alifika na wenzake kwa lengo la
kufundishwa kuogelea lakini kilichompata hatasahau.“Mimi kila wakati
nikienda kule beach natamani sana kuogelea lakini nilikuwa siwezi ndo
nikaambiwa wale vijana wanaokodisha yale maboya ukitaka
wanakufundisha.“Siku moja nikaenda pale, nikaongea na kijana mmoja
ambaye alikubali kunifundisha kwa malipo ya shilingi elfu tano. Wakati
ananifundisha akawa ananipeleka kwenye sehemu yenye maji mengi, tukaenda
mbali sana ambako nisingeweza kurudi peke yangu.“Huko akaanza kunitaka
nimpe penzi huku akisema hata nisipomlipa, kwa kweli nilichangayikiwa.
Wakati najifikiria alishaanza kunichezea kisha akanibaka,” alidai binti
huyo.
OFM KAZINI
Baada ya kupata madai hayo, makamanda wa OFM
wikiendi iliyopita walitinga katika eneo hilo na kukuta vijana
wakiendelea na zoezi la kuwafundisha kuogelea watu mbalimbali, asilimia
kubwa wakiwa ni wanawake.Katika uchunguzi uliofanyika ilibainika kuwa,
kuna uwezekano mkubwa wa vitendo vya ubakaji kuchukua nafasi kwenye
zoezi hilo kutokana na mazingira yalivyo.Akizungumzia tuhuma hiyo, mmoja
wa ma-beach boys aliyejitambulisha kwa jina la Faridi alisema: “Unajua
tunaofanya kazi hii tuko wengi na kila mmoja ana tabia zake, hivyo
siwezi kukataa kuwa vitendo hivyo havipo.
“Ila wakati mwingine hawa
tunaowafundisha wanatupa mtihani kwa mavazi yao na ‘viuchokozi’ vyao,
sasa sisi kama wanaume tuliokamilika wakati mwingine inakuwa ngumu
kuvumilia,” alisema kijana huyo.
POLISI WAWAFUNGIA KAZI
Kufuatia
vitendo vya ubakaji kushamiri maeneo hayo, jeshi la polisi hivi karibuni
lilifanya doria na kuwakamata watu 33 wakiwemo ‘Beach Boys’ huku
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro akisema
kuwa watuhumiwa hao wamenaswa baada ya askari kufanya msako na kukutwa
wakifanya mapenzi kwenye Ufukwe wa Bahari ya Hindi.
TAHADHARI
Gazeti
hili linapenda kuwatahadharisha wazazi na mabinti zao kuwa makini na
vijana hao ambao wameonekana kuwa tatizo. Epuka kufundishwa kuogelea na
mtu ambaye humjui na wala huna imani naye.
CHANZO: GAZETI LA RISASI JUMATANO
0 comments:
Post a Comment