Mwandishi wetu, Risasi Jumamosi
MPANGO
au matarajio ya kila mwanadamu ni kuishi katika uchumba, kuolewa kisha
kupata watoto! Wapo ambao wamefanikiwa hilo, wapo ambao wamepata kwanza
mimba baadaye wakaolewa lakini wapo pia waliopata mimba kabla ya ndoa
kisha wakatofautiana na waliowapa, kila mmoja anaishi kivyake.
Katika
ulimwengu wa mastaa wa kike Bongo, leo nakuletea baadhi ya mastaa ambao
wamepata watoto lakini kwa namna moja au nyingine safari yao na
waliowapa ujauzito haikufika mbali, ikavunjika. Wapo ambao walipata
kabla na wengine baada ya ndoa.
Wengi
wao huwanadi watoto hao mitandaoni kwa maneno mazuri wakionesha kwamba
ndiyo faraja yao baada ya kuachana na wapenzi au waume wao;
ROSE NDAUKA
Aliingia
katika uchumba na Malick Bandawe. Wakafanikiwa kupata mtoto mmoja,
uchumba ukayeyuka wakati wawili hao wakiwa katika mchakato wa kuelekea
kwenye ndoa.
SNURA MUSHI
Amefanikiwa
kupata watoto wawili; wa kike na wa kiume kwa baba tofauti. Wote
wameingia mitini. Akapata mchumba mpya, naye wakamwagana kabla ya
kufanikiwa kuolewa wala kuzaa.
ZUWENA MOHAMMED ‘SHILOLE’
Ana
watoto wawili wa kike ambao alizaa na wanaume wawili tofauti kwa
nyakati tofauti. Kwa sasa wamemuachia chata ya watoto hao wa kike ambao
anawadi mitandaoni.
KAJALA MASANJA
Aliingia
kwenye ndoa na Faraji Agustino akiwa tayari ameachiwa chata moja ya
kike na Prodyuza, Paul Matthysse ‘P Funk’. Bahati mbaya mumewe
hakufanikiwa kuzaa naye, akafungwa kwa msala wa kutakatisha fedha
haramu. Hadi sasa ana furaha kuwa na binti yake huyo.
HAMISA MOBETO
Alikuwa
kwenye uchumba na bosi wa redio moja maarufu, akafanikiwa kupata mtoto
mmoja na uchumba ukaishia hapo. Kila mtu yupo kivyake kwa sasa Mobeto
anajifariji na chata yake ya kike aliyoachiwa.
JENIFFER KYAKA ‘ODAMA’
Inasemekana
amezaa na kigogo mmoja ambaye ana familia yake. Inadaiwa kuwa kigogo
huyo ameelekeza nguvu zake kwa mkewe hivyo Odama kubaki na chata yake
ambayo anainadi kwenye mitandao ya kijamii mara kwa mara.
IRENE UWOYA
Aliingia
kwenye ndoa na mshambuliaji wa zamani wa Rayon Sports ya Rwanda, Hamad
Ndikumana ‘Katauti’. Akafanikiwa kupata mtoto mmoja wa kiume (Krish)
kisha ndoa ikasambaratika na sasa anafarijika kwa kuachiwa kopi yake.
WENGINE
Masta
wengine ambao kwa namna moja au nyingine wamezalishwa na kuachiwa
watoto ni pamoja na Shamsa Ford, Faiza Ally aliyezaa na Mbunge wa Mbeya
Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’, Siwema Edson (aliyekuwa demu wa Nay wa
Mitego) na Riyama Ally ambaye ameachiwa chata ya kike.
0 comments:
Post a Comment