Friday, January 13, 2017

Jana January 11 katika kipindi cha Ala za Roho cha Clouds FM hitmaker wa ngoma ya Muziki Darassa CMG alikuwa mgeni rasmi katika kipindi hicho kwaajili ya kufanyiwa interview na Diva The Bawse ambaye ndio host wa kipindi hicho.
Maswali ni mengi ambayo aliulizwa mkali huyo lakini moja kati ya hayo ni kwamba amewahi kwenda kwa Mganga wa kienyeji!
“Kwenye maisha yangu nimeshawahi kwenda kwa mganga zamani sana, sisi tunaoishi uswahilini ni vitu vingi vinatokea. Nilikwenda kwa nia ya kuji-google tu, haikuwa inahusiana kabisa na music, ni personal life yangu.” Alisema Darassa.
Swali kwako wewe msomaji, umewahi kwenda kwa mganga? Niandikie hapa chini na uniambie ni sababu gani zilikupeleka kwa mganga huyo.

0 comments:

Post a Comment