Ikiwa ni wiki chache tu zimepita tangu itangazwe list ya video za muziki Africa ambazo zimetazamwa mara nyingi zaidi katika mtandao wa Youtube kwa mwaka 2016 na video ya Salome ya Diamond Platnumz na Rayvanny kushika nafasi ya pili, Diamond Platnumz ameitaja ngoma ambayo kwa mtazamo wake anaona imefanya vizuri zaidi Africa kuliko ngoma zake zote.
Pamoja na mafanikio yote hayo ya wimbo wa Salome, Diamond Platnumz ameutaja wimbo wa Kidogo ambao kafanya na P-Square kuwa ndio wimbo ambao anaona umefanikiwa zaidi kimataifa kuliko ngoma zake zote.

Diamond Platnumz amefunguka hayo wakati akifanya interview na Sports Extra ya CLouds FM usiku wa jana ikiwa ni katika hali ya kuzungumzia mapokezi yake kwenye show ambayo aliifanya kwenye ufunguzi wa kombe la mataifa ya Africa (AFCON) huko nchini Gabon.
“Ukiangalia nyimbo ambayo nimefanya na P-Square kinyumbani haijafanya vizuri kulinganisha na nyimbo kama Salome, lakini ni nyimbo ambayo imefanya vizuri Africa kuliko nyimbo zangu zote za sasa hivi naweza kusema. Ndio nyimbo ambayo inanipa chanel nyingi sana katika kila nchi ninayoenda kuliko hata nyimbo zote ambazo nimewahi kuzifanya.” Alisema Diamond Platnumz.
Unaweza kuisikiliza full interview ambayo ameifaya Diamond Platnumz na Sports Exter ya Clouds FM kwa kuplay hii video hapa chini.
0 comments:
Post a Comment