Ukizungumzia vitu ambavyo vime make headlines kinoma noma weekend hii huwezi kuacha kuitaja show ambayo aliifanya Diamond Platnumz kwenye ufunguzi wa michuano ya AFCON huko nchini Gabon jumamosi iliyopita.
Wengi walienjoy kwa show hiyo lakini kilicho washangaza wengi ni ule wimbo ambao Diamond Platnumz aliperform na msanii wa kimataifa wa Sweeden afahamikae kama Mohombi!
Ni wimbo ambao ulikuwa mgeni katika masikio ya wengi na maswali mengi yalijitokea kuhusu wimbo huo kwenye performance ya wakali hao ukizingatia walikuwa wakienda sawa hadi kwa steps za uchezaji wa wimbo huo.
Sasa ni official Diamond Platnumz ametusanua kuhusiana na wimbo huo kwamba wapo nchini Gabon kushoot baadhi ya vipande vya video ya wimbo huo ambao ni remix ya wimbo ambao unaitwa Rockonolo na kisha jumanne kuja kumalizia vipande vingine hapa Tanzania.
Ni kupitia ukurasa wake wa Instagram ndio sehemu ambayo Diamond Platnumz ametusanua maunyama hayo.

0 comments:
Post a Comment