Moja kati ya story zilizo trend kinoma kwa mwaka 2016 ni pamoja na bifu zito la malegendary wa muziki wa Bongo Fleva TID na Prince Dully Sykes.
Bifu ambalo chanzo chake inasemekana kuwa ni Dully Sykes kukataa kutokea kwenye kichupa cha wimbo wa confidence. Wimbo ambao unamilikiwa na T.I.D ikiwa audio version yake Dully Sykes pamoja na Joh Makini wapo humo ndani.
Mengi yaliongelewa lakini Dully Sykes hakuwahi kusikika hata kwenye interview moja kulizungumzia suala hilo. Leo kwa mara ya kwanza mkali huyo amefunguka kupitia kipaza cha Perfect255 kuhusiana na bifu hilo.
“Kiukweli mimi TID namchukulia kama rafiki yangu, japo tunaweza kukutana tusiongee lakini mimi huwa sina kinyongo na mtu. Amenisema , amenizungumzia vibaya, lakini TID atabaki kuwa TID rafiki yangu wa zamani, nitamthamini. Siwezi kumkuta TID anapata kitu kibaya mimi nikafurahia hata siku moja. Mimi namuombea maisha mazuri tu na pia namuombea apate kurudi tena kwenye game ili nipate hata mpinzani.” Alisema Dully Sykes.
Dully Sykes alikanusha taarifa zinazodai kuwa bifu hilo lilisababishwa na Joh Makini kuwepo kwenye ngoma ya confidence bila kufahamishwa na akadai kuwa walikorofishana na TID kwenye kushoot video hiyo na ndio maana hakutokea kwenye kichupa hicho.

0 comments:
Post a Comment