Wasanii wa muziki na filamu wamepata nafasi ya kuwepo tena ndani ya Ikulu ya Marekani katika sherehe ndogo ya kumuaga Rais Barack Obama Ijumaa hii ya Januari 6.
Ikulu ya Marekani imesema sherehe hiyo itafanyika kwenye viwanja vya Ikulu hiyo ambapo Rais Obama na mkewe Michelle Obama wanatakuwa washereheshaji.
Mastaa walioalikwa kwenye sherehe hio ni pamoja na Beyoncé, Jay Z, Stevie Wonder, Usher, Oprah Winfrey, Samuel L. Jackson, Bradley Cooper, George Lucas.
Obama anatarajia kumkabidhi rasmi madaraka ya kuiongoza nchi hiyo Donald Trump Januari 20 baada ya kumaliza miaka minane ya uongozi wake.
0 comments:
Post a Comment