Saturday, January 21, 2017

Tumekuwa tukisikia stori za treni zenye kasi kuzinduliwa maeneo mbalimbali duniani kama vile China, sasa taarifa iliyotolewa January 2017 imeeleza kuwa treni ya kwanza na yenye kasi zaidi Afrika itaanza kutumika Morocco.

Unaambiwa treni hiyo ina uwezo wa kuzimaliza kilometa 321 kwa saa ambapo kwa harakaharaka ingekua Tanzania inaweza kufika Arusha ikitokea Dar kwa dakika zisizofika 120.
Pesa iliyotumika kwenye huu mradi ni Dola za kimarekani BILIONI 2, ni pesa ndefu ambayo imepatikana baada ya mradi huo kuwekewa mikono na nchi 6, serikali ya Morocco yenyewe, Ufaransa, Saudi Arabia, Kuwait, na UAE.

0 comments:

Post a Comment