Tumeshuhudia maproducer kibao bongo wakiwa na maproducer wengine wadogo katika kusaidia kazi zao, ila kwa upande wa P Funk Majani jambo hili ni tofauti kutokana na kuogopa kuharibiwa vyombo alafu mwisho wa siku wasilipie.
P Funk Majani ni moja ya malegendary katika industry hii ya maproducer Bongo, Sasa kama kawaida waya wa Perfect255 ukamnasa P Funk ilikujua kwanini yeye ameamua kukomaa kwenye game hii bila kuwa na wasaidizi wengine nazungumzia maproducer wadogo ambao watasaidia kuongeza maujanja ndani ya kazi yake.
Akiongea na Perfect255, P Funk Majani alifunguka kwa kusema kwamba hawezi kuwaachia kwani anaogopa kuharibiwa vifaa vyake vya studio
“Sasa uwape ili wafanye nini waniharibie vyombo alafiu hela isiingie, unajua kitu ukiachia ….unapokuwa umenunua dala dala, unajua kabisa hii itanirudishia hela ili nifanye matengenezo, nipate faida, kama kikishaharibika nitakuwa na uwezo wa kununua Dala dala nyingine, sasa wewe utanunua dala dala alafu usiweke tiketi wawe wanatembea bure tu, gari linachakaa tu alafu bila kufanyiwa service, sasa ningefungua studio watu wangekuwa wanarekodi lakini hakuna masilahi ya kulipia luku, hakuna masilahi ya kununua spika mpya ukiharibu au computer mpya” Alifunguka P Funk.
0 comments:
Post a Comment