“Habari
mpya ni kwamba Diamond Platnumz atakuwa mgeni rasmi katika pati ya Zari
All White Ciroc, najihisi niko sahihi kwa sababu sioni kama kuna
ushindani wowote, huyu ni mtu wangu na itabaki kuwa hivyo,”
Johannesburg/Dar.
Baada ya kuukimbia ukweli kwa kipindi cha mwezi mmoja, mwanamuziki
Diamond Platnumz amethibitisha kuwa na uhusiano baina yake na staa
maarufu kutoka Uganda, Zari ‘The Boss Lady’ na kwamba atakuwa mgeni
rasmi katika hafla yake ijulikanayo ‘Zari All White Ciroc’
itakayofanyika mwezihuu.
Nyota
huyo aliyevunja rekodi kwa kunyakua tuzo tatu za Channel O Music Video
Awards (ChoMVA) wikiendi iliyopita, amekuwa akijadiliwa katika mitandao
ya Tanzania na nje ya nchi kwa kuonekana na wanawake tofauti kila
wakati, hali inayowachanganya mashabiki wake. Hata hivyo, Diamond
hajasita kuelezea hisia zake za sasa na kwamba yupo tayari kuhudhuria
hafla hiyo, inayotarajiwa kufanyika Desemba 18. “Nitakuwapo katika hafla
hiyo, ni lazima nimuunge mkono, mbona kuna wengi wanaunga mkono na watu
hawasemi, kama wanavyokaa kimya kwa wengine nahuku iwe vivyo hivyo,”
alisema Diamond huku akishindwa kukiri moja kwa moja kwamba ana uhusiano
na Zari, “waswahili wanasema A na B yote majibu.”>>>
0 comments:
Post a Comment