Thursday, January 12, 2017

3x6a9453 Huu ndio muonekano wa nje wa iliyokuwa ngome ya utawala wa Ureno wakati wa ukoloni. Ngome hii inapatikana kwenye visiwa vya Mombasa nchini Kenya, iko umbali wa kilomita 490 kutokea jiji la Nairobi.

Fort Jesus (Ngome ya Yesu), ilijengwa na wakoloni wa Kireno kuanzia mwaka 1593 hadi 1596 ikiwa na ramani iliyochorwa na mbunifu wa majengo “Giovanni Battista Cairati” kwa lengo la kulinda bandari ya Mombasa, ngome hii inafananishwa na ngome za taifa la Ureno zilizokuwepo karne ya 16 zikitumiwa na jeshi la nchi hiyo.
Ukubwa wa eneo ilipojengwa ngome hiyo unatajwa kufikai hekta 2.36 zikijumisha eneo la majengo na mazingira yake.
3x6a9460 3x6a9445 3x6a9456 3x6a9452 3x6a9451 3x6a9447 3x6a9448 3x6a9449 3x6a9450

0 comments:

Post a Comment