Msanii wa muziki wa hip hop, Nay wa Mitego amemtambulisha producer mpya wa studio yake Free Nation Record baada ya kuachana na Mr T Touch.
Rapper huyo ameonekana akiwa studio na producer huyo aitwae Osam wakirekodi wimbo mpya.
Producer huyo kupitia taarifa aliyoitoa kupitia Instagram, amedai amesainiwa studio hiyo ya Free Nation Record kama producer wa studio.
Nay wa Mitego na Mr T Touch wanadaiwa kuachana baada ya kushindwana kibiashara ambapo kwa sasa producer huyo amefungua studio mpya iliyopo Sinza Jijini Dar es salaam. Angalia picha za studio hiyo.
Nay wa Mitego akiandaa kazi mpya ndani ya studio hiyo
0 comments:
Post a Comment