Saturday, January 28, 2017

Baada ya kulalamika juu ya video yake ya “Hela” kutoweka kwenye chaneli yake ya Youtube, Madee amerudi upya na kusema kwamba waliomfanyia tukio hilo atawaanika katika kurasa yake.

“Hela” ni moja ya ngoma ambayo bado inasumbua kila kona kwenye masikio ya watu kila inapopigwa, Bad newz ni kwamba tangu siku moja kupita baada ya Madee kufunguka kuhusu video ya wimbo huo kufutwa, leo amerudi upya na mapovu kwa wale ambao waliomfanyia hivyo na kikubwa ni kwamba ameahidi kuwaweka hadharani kwani namba zao anazo.

Kupitia kurasa yake ya Instagram, Madee aliamua kufunguka kwa kusema kwamba baada ya kushindwa mchezo wa hadharani sasa wanaleta janja janja kwa kuirepot kazi yake kuwa ina matatizo.
Baada ya kushindwa mchezo wa hadharani sasa mnaleta janjajanja ya michezo yenu michafu/et unairepot kazi isiokuhusu youtube itolewe kua una matatizo nayo..mbona mnatumia nguvu nyingi sana kwenye hili..haya imetolewa toka juz nini umefaidika!!mnataka muwe nyinyi tu kila siku oooh sio fair kabisa!!! TAARIFA video ya hela imefutwa na youtube na kipindi inafutwa ilikua nisiku tatu toka itoke na tayari ilikua ndio NO1 youtube na tayari ilikua na viewers 357,109  Tumeangaika na tumefikia pazuri na kuwabain watu waliofanya huo mchezo so nitawataja soon na no zao tutaziweka apa// wase…….. laaaaaa #WinoMweusi

0 comments:

Post a Comment