Saturday, January 7, 2017

Rapa Kala Jeremiah amefunguka na kusema siku zote safari ya mtu ambaye anatumia madawa ya kulevya ni nyeupe na mwisho wake ni kupoteza uhai wake mwenyewe kwani hakuna njia ambayo inaweza kumsaidia kama hataweza kuacha na matumizi ya dawa hizo.

Kala Jeremiah alisema hayo eNEWZ ya EATV na kusema yeye anaamini wazi kuwa kama serikali itaamua kuwakamata watu wanaofanya biashara ya dawa za kulevya ni rahisi sana kwa kuwakamata watumiaji na kuwabana vilivyo watasema wapi wananunua hizo dawa.
"Mimi siamini kama watu wanaouza madawa ya kulevya wanashindikana kukamatwa kwa sababu ukimkamata huyo teja ukimbana vizuri atakupeleka kwa pusha na pusha ukimkamata ukamtaiti vizuri atasema anatoa wapi hizo dawa. Watu wanatakiwa kujua dawa za kulevya ni sumu haina mwisho mwingine zaidi ya kaburi, yaani hakuna mwisho mwingine wa mtu anayetumia madawa ya kulevya zaidi ya kufa kwani kifo chake kimenyooka hakuna kupinda pinda" alisema Kala Jeremiah 

0 comments:

Post a Comment