
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira akipewa maelezo na Meneja Uzalishaji wa Kiwanda cha Urafiki kilichopo jijini Dar es Salaam Thomas Mushi, juu ya bidhaa zinazozalishwa na Kiwanda hicho alipofanya ziara ya kikazi akiwa ameambatana na maofisa wa majeshi yaliyo chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ili kujionea ubora wa bidhaa zinazozalishwa viwandani humo kwa kuwa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi inategemea kuanza kuagiza vitambaa vya sare za Majeshi yake kutoka viwanda vilivyopo nchini hapa.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira akioneshwa hatua za awali za namna pamba inavyoandaliwa katika Kiwanda cha Urafiki kilichopo jijini Dar es Salaam kabla ya kutengeneza bidhaa. Katibu Mkuu huyo alitembelea kiwanda hicho akiambatana na baadhi ya maofisa wa majeshi yaliyopo chini ya wizara yake (hawapo pichani) ili kujionea ubora wa bidhaa zinazozalishwa kiwandani humo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira akioneshwa jinsi mitambo iliyopo katika kiwanda cha Urafiki inavyofanya kazi katika uzalishaji wa bidhaa zinazotoka kiwandani hapo na Salum Dailuga ambaye ni Meneja utiaji rangi na uchapishaji wa bidhaa. Wa kwanza kulia ni Kamanda wa Polisi Kamishna Msaidizi wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Ilala Hamdan Salum aliyeambatana na Katibu Mkuu huyo kwenye ziara hiyo iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira pamoja na Maofisa mbalimbali wa majeshi yaliyopo chini ya wizara hiyo wakitazama khanga iliyozalishwa kiwanda cha Urafiki wakati alipotembelea kiwanda hicho ili kujionea ubora wa bidhaa zao.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira akioneshwa malighafi iliyopo katika hatua za mwishoni kabla ya kwenda kutengenezwa mashuka katika kiwanda cha NIDA Textile MILLS (T) LTD, kilichopo Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam ambako alitembelea leo pamoja na baadhi ya maofisa wa majeshi yaliyopo chini ya Wizara hiyo, kwa lengo la kujionea ubora wa bidhaa zinazozalishwa viwandani humo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira akiangalia mfano wa vitambaa vinavyozalishwa na kiwanda cha NIDA Textile MILLS (T) LTD kilichopo maeneo ya Tabata jijini Dar es Salaam ambako alitembelea leo pamoja na baadhi ya maofisa wa majeshi yaliyopo chini ya Wizara hiyo, kwa lengo la kujionea ubora wa bidhaa zao.
Baadhi ya maofisa wa Majeshi yaliyo chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi waliokuwa wameambata na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (Hayupo pichani), wakiwa na sampuli zao za vitambaa vya sare zao.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira akielekea katika maeneo ambayo Kiwanda cha Urafiki kilichopo jijini Dar es Salaama kinazalisha bidhaa zake. Katibu Mkuu huyo alitembelea kiwanda hicho leo akiwa na baadhi ya maofisa wa majeshi yalipo chini ya wizara yake kwa ajili ya kuangalia ubora wa bidhaa zinazozalishwa viwandani humo.Mwenye suti nyeusi ni Shedrack Mkelebe ambaye ni Naibu Meneja Mkuu wa kiwanda hicho. Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi inategemea kuanza kuagiza vitambaa vya sare za Majeshi yake kutoka viwanda vilivyopo hapa nchini.
……………
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira amefanya ziara katika Viwanda vya NIDA na Urafiki vinavyotengeneza nguo vilivyopo jijini Dar es Salaam. Lengo la ziara hii ni kuangalia ubora wa bidhaa zinazozalishwa viwandani humo kwa kuwa Wizara inategemea kuanza kuagiza vitambaa vya sare za Majeshi yaliyopo ndani ya wizara hii kutoka viwanda vilivyopo hapa nchini.
Katika ziara hii Meja Jenerali Rwegarisa aliambatana na baadhi ya maofisa wa majeshi yaliyopo chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi wakiwa na sampuli za aina za vitambaa wanavyohitaji kwa ajili ya sare za majeshi yaliyoko chini ya wizara hii.
Uamuzi wa Ofisi ya Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kuwafuata watengenezaji moja kwa moja na hivyo kuacha kutumia wazabuni kutapunguza gharama zilizokuwa zikiongezwa na mtu wa kati. Mbali ya Viwanda alivyotembelea bado atatembelea viwanda vingine vilivyopo mikoani kama vile Arusha, Mwanza na Morogoro.
Aidha viwanda vya ndani vitainuliwa kwa kuviunga mkono kwani bidhaa zinazozalishwa na viwanda vya ndani zina ubora mzuri hivyo kuzifanya hata nchi za jirani mfano Kenya na Zambia kuendelea kuagiza bidhaa kutoka viwanda vya hapa nchini.
Hata hivyo, viwanda vya ndani vya kutengeneza nguo vinaweza kupewa zabuni bila upendeleo wowote kitakachoangaliwa ni ubora wa bidhaa zinazozalishwa kama zinakidhi mahitaji ya sare za majeshi yaliyopo chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Imetolewa na
Christina R. Mwangosi
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
0 comments:
Post a Comment