Posted by Williammalecela.com on Saturday, January 14, 2017
Kama unamfatilia Zari katika mitandao ya kijamii wiki chache zilizopita utakuwa umekutana na post ya picha ya mpenzi wake wa zamani ikiwa ni kama kumpa support kwenye party iliyokuwa inafanyika Uganda
Diamond kupitia amplifaya ya Clouds Fm amefunguka jinsi anavyojisikia pale ambapo zari ambaye ni mama wa watoto wake sasa hivi anapo'post picha ya mpenzi wake wa zamani ambae ni ivan
"Watu wanashindwa kuelewa lazima ujiamini kwenye mahusiano yako yule ni mzazi mwenzake alizaa nae hawakuoana kwanza watu wajue, hawajawahi kuoana walikuwa ni wapenzi wamezaa, kwahiyo kuwa na mimi haimaanishi yule ndio adui yake hapana, japokuwa kuna vitu vya muhimu kama ana shughuli yake anatakiwa amsupoti anamsapoti, kama let say kuna maswala ya watoto wanatakiwa wazungumze" alisema Diamond kwenye amplifaya ya Millard ayo muda mchache uliopita
"ina maana ukiweka hivyo inabidi kesho na kesho kutwa mimi labda nikiongea na wema au nikiongea na mtu yeyote Zari achukie..? hawezi kuchukia, so nikutumia akili zaidi kuliko kufikilia negativity" aliongeza
0 comments:
Post a Comment