Friday, January 6, 2017

Msanii wa bongo fleva Mh.Temba amesema majukumu ya kuongoza makundi mbalimbali ikiwemo Yamoto Band  pamoja na TMK Wanaume ndo vilipelekea kushindwa kutoa nyimbo nyingi mwaka 2016.

Akiongea kupitia eNewz Temba amesema muziki kwa sasa ni biashara hivyo unapoamua kufanya nyimbo inabidi uweke pesa ya kutosha ili ukiachia nyimbo iweze kufanya vizuri na kurudisha pesa iliyotumika na pia tuweze kuwaridhisha mashabiki zetu kwa njia tofauti.
Hata hivyo Temba amewaomba radhi mashabiki zake ambao walikosa burudani za nyimbo zake kwa mwaka 2016 na kusema kwa sasa anajipanga ili kuweza kufanya nyimbo nzuri kwa mwaka 2017 kwa kuwa bado yeye ni Temba na hakuna kilichobadilika kwake. 

0 comments:

Post a Comment