Friday, January 13, 2017

Wakati akiwa kwenye maandalizi kwa ajili ya pambano lake na Chris Brown, Soulja Boy mjengo wake ulivamiwa huko Hollywood.

Kupitia mtandao wa Tmz umeripoti kwamba mjengo wa Soulja Boy uliopo Hollywood ulivamiwa na mhuni mmoja na kufanikiwa kuondoka na mtonyo wa dola $10,000 pamoja na vito vya thamani vyenye gharama ya dola $12,000, tukio hilo lilifanyika pindi Soulja Boy hayupo mjengoni mwake.
Good Newz ni kwamba Camera ambazo zilikuwepo zilifanikiwa kupata picha ya mwizi huyo na polisi ndio wapo kwenye uchunguzi wa kumtafuta, baadhi ya mashabiki wamekuwa wakifunguka na kusema kwamba nteramefanyiwa hivyo ni baada ya kujigamba kwenye mahojiano yake na  VladTV kwamba alishawahi kuwapiga risasi vibaka ambao walikuwa wamevamia nyumbani kwake.
Licha ya wawili hao kujiandaa kwenda kwenye pambano lao Huko Dubai, hakuna taarifa ambayo imetolewa kama wizi huo umesababishwa na ugomvi wao kati yake Soulja boy na Chris Brown.

0 comments:

Post a Comment