Thursday, January 26, 2017

Msanii wa filamu Ben Selengo amesema kwa sasa anaendelea vizuri ikiwa ni mwezi mmoja toka apate ajali mbaya ya gari Disemba 25 mwaka jana.

Akiongea na Bongo5  Ben amesema kwa sasa anauguza majeraha ambayo aliyapata katika ajili hiyo ambayo ilimpelekea kulazwa Muhimbili kwa wiki kadhaa.
“Mungu ni mwema kabisa sasa hivi naendelea vizuri japokuwa sijaanza kazi,” alisema Ben. “Nikiendelea hivi hivi soon nitaingia mgigoni tena kwa sababu sasa hivi kuna majeraha ambayo yanamalizia kukauka,”
Muigizaji huyo ambaye pia ni producer wa filamu amedai ndani ya mwezi ujao anadhani atakuwa fit kabisa tayari kwa kurejea kazini.

0 comments:

Post a Comment