Kama upo kwenye Industry ya muziki wa HipHop hapa Bongo na hauna attitude ya HipHop wala mistari kwenzi basi hauwezi kuingia kwenye listi ya ngoma anazopenda kusikiliza Mhe. Dr. Hamis Kigwangalla
Baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mh Paul Makonda kufunguka kuhusu Fid Q kwenye ngoma ya Roho, Naibu waziri wa Afya Mhe. Dr. Hamis Kigwangalla ameamua kushuka baadhi ya michano ya Fid q.
Kupitia mfululizo wa Tweets za Mhe. Dr. Hamis Kigwangalla, ameonekana kuguswa na mistari ya Fid Q, kutoka kwenye video ya wimbo wa Kemosabe, huku akifunguka kwa kusema kwamba huwa anawasikiliza sana wasanii wachache wa Bongo Fleva, ambapo Fid Q ni moja wapo wa hao kutokana na uwezo wake wa kuandika mistari pamoja na attitude ya Hiphop.
Huwa nasikiliza wasanii wachache sana wa Bongo flavour, @FidQ ni mmojawapo, sababu anajua kutunga mistari na ana attitude ya hip-hop!

0 comments:
Post a Comment